Surat Al-An'am, aya 58

6:58

قُل لَّوۡ أَنَّ عِندِي مَا تَسۡتَعۡجِلُونَ بِهِۦ لَقُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ بَيۡنِي وَبَيۡنَكُمۡۗ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِٱلظَّٰلِمِينَ ٥٨

Qul law anna 'indī mā tasta'jilūna bihī laqudiyal-amru baynī wabaynakum wallāhu a'lamu biz-zālimīn

Sema: Lau kuwa ninacho hicho mnacho kihimiza, ingeli kwisha katwa shauri baina yangu na nyinyi. Na Mwenyezi Mungu anawashinda wote kuwajua madhaalimu. 58

Maelezo ya chini

58 Sema: Lau ingeli kuwa kumo katika makadara yangu kukuteremshieni hiyo adhabu mnayo ihimiza ije, ningeli kuteremshieni kwa kukasirika kwa ajili ya Mola Mlezi wangu. Na hapo mambo yangeli kwisha baina yangu na nyinyi. Walakini amri ni ya Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mwenye kujua kuliko wote wanayo stahiki makafiri katika adhabu ya haraka, au ya kuakhirika.