Surat Al-An'am, aya 26

6:26

وَهُمۡ يَنۡهَوۡنَ عَنۡهُ وَيَنۡـَٔوۡنَ عَنۡهُۖ وَإِن يُهۡلِكُونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡ وَمَا يَشۡعُرُونَ ٢٦

Wahum yanhawna 'anhu wayan'awna 'anhu wa in yuhlikūna illā anfusahum wamā yash'urūn

Nao huwazuia watu, na wao wenyewe wanajitenga nayo. Nao hawaangamizi ila nafsi zao tu, wala wao hawatambui. 26

Maelezo ya chini

26 Wao huwazuia watu wasiiamini Qur'ani, na wao wenyewe hujitenga nayo. Inakuwa wao hawanafiiki, wala hawawachii wenginewe wakanafiika! Na kwa kitendo hicho hawadhuru ila nafsi zao, na wao hawatambui ubaya wa wayatendayo.