Surat Al-An'am, aya 164

6:164

قُلۡ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ أَبۡغِي رَبّٗا وَهُوَ رَبُّ كُلِّ شَيۡءٖۚ وَلَا تَكۡسِبُ كُلُّ نَفۡسٍ إِلَّا عَلَيۡهَاۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٞ وِزۡرَ أُخۡرَىٰۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرۡجِعُكُمۡ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ فِيهِ تَخۡتَلِفُونَ ١٦٤

Qul aghayrallāhi abghī rabban wahuwa rabbu kulli shay'in walā taksibu kullu nafsin illā 'alayhā walā taziru wāziratun wizra ukhrā thumma ilā rabbikum marji'ukum fayunabbi'ukum bimā kuntum fīhi takhtalifūn

Sema: Je nitafute Mola Mlezi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ndiye Mola Mlezi wa kila kitu? Na kila nafsi haichumii ila nafsi yake. Na habebi mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi, naye atakuambieni mliyo kuwa mkikhitalifiana. 164

Maelezo ya chini

164 Sema ewe Muhammad, kuwakatalia washirikina wito wao kwako, uwakubalie ushirikina wao: Nimtafute wa kumuabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ndiye Muumba wa kila kitu? Na waambie kuwakatalia kuwa wao hawawezi kukubebea makosa yako ikiwa utawakubalia: Hapana nafsi inayo tenda kitu ila itapata malipo yake wenyewe peke yake. Hachukui mtu dhambi za mwenziwe. Kisha mtafufuliwa kwa Mola Mlezi wenu baada ya mauti, naye atakupeni khabari ya hayo mliyo khitalifiana kwayo duniani, katika mambo ya itikadi, na atakulipeni kwayo. Basi vipi nimuasi Mwenyezi Mungu kwa kutegemea ahadi yenu ya uwongo.