لَا شَرِيكَ لَهُۥۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرۡتُ وَأَنَا۠ أَوَّلُ ٱلۡمُسۡلِمِينَ ١٦٣
Lā sharīka lahū wabidhālika umirtu wa ana awwalul-muslimīn
Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu. 163
Maelezo ya chini
163 Hana mshirika katika kuumba, wala katika kustahiki kuabudiwa. Naye Yeye Mola Mlezi wangu ameniamrisha kwa hayo nimfanyie ikhlasi (usafi wa niya) katika Tawhidi (kutakasisha upweke wake) na vitendo. Na mimi ni wa kwanza wa kumnyenyekea, kumfuata, na mkamilifu wao wa ut'iifu na kusilimu.