Surat Al-An'am, aya 162

6:162

قُلۡ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحۡيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٦٢

Qul inna salātī wanusukī wamahyāya wamamātī lillāhi rabbil-'ālamīn

Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote. 162

Maelezo ya chini

162 Sema: Hakika Sala yangu na ibada zangu, na niyafanyayo katika hali ya uhai wangu, nayo ni ut'iifu, na Imani na vitendo vyema ninavyo kufa navyo, vyote hivyo nimevisafia kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu Aliye umba vitu vyote, na kwa hivyo akastahiki kuabudiwa Yeye peke yake, na kut'iiwa Yeye peke yake.