قُلۡ إِنَّنِي هَدَىٰنِي رَبِّيٓ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ دِينٗا قِيَمٗا مِّلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۚ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ ١٦١
Qul innanī hadānī rabbī ilā sirātim mustaqīmin dīnan qiyamam millata ibrāhīma hanīfan wamā kāna minal-mushrikīn
Sema: Kwa hakika mimi Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka, Dini iliyo sawa kabisa, ambayo ndiyo mila ya Ibrahim aliye kuwa mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina. 161
Maelezo ya chini
161 Sema ewe Nabii kwa kubainisha Dini ya Haki unayo ifuata: Hakika Mola wangu ameniongoza, na ameniwafikisha kuishika Njia Iliyo Nyooka, yenye kufika ukomo wa kukamilika na kunyooka. Na Dini hii ndiyo aliyo ifuata Ibrahim akaacha itikadi zote potovu. Na Ibrahim hakuwa akimuabudu mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, kama wanavyo dai washirikina.