مَن جَآءَ بِٱلۡحَسَنَةِ فَلَهُۥ عَشۡرُ أَمۡثَالِهَاۖ وَمَن جَآءَ بِٱلسَّيِّئَةِ فَلَا يُجۡزَىٰٓ إِلَّا مِثۡلَهَا وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ ١٦٠
Man jā'a bil-hasanati falahū 'ashru amthālihā waman jā'a bis-sayyi'ati falā yujzā illā mithlahā wahum lā yuzlamūn
Afanyae wema atalipwa mfano wake mara kumi. na afanyae ubaya hatalipwa ila sawa nao tu. Na wao hawatadhulumiwa. 160
Maelezo ya chini
160 Mwenye kutenda mema atalipwa thawabu zake mpaka mara kumi kwa kufadhiliwa na kukirimiwa. Na mwenye kutenda ovu hatoadhibiwa ila kwa kadri ya maasi yake tu, kwa uadilifu wake Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na hapo hapana dhulma kwa kumpunguzia mtu thawabu, wala kumzidishia adhabu.