Surat Al-An'am, aya 156

6:156

أَن تَقُولُوٓاْ إِنَّمَآ أُنزِلَ ٱلۡكِتَٰبُ عَلَىٰ طَآئِفَتَيۡنِ مِن قَبۡلِنَا وَإِن كُنَّا عَن دِرَاسَتِهِمۡ لَغَٰفِلِينَ ١٥٦

An taqūlū innamā unzilal-kitābu 'alā tā'ifatayni min qablinā wa in kunnā 'an dirāsatihim laghāfilīn

Msije mkasema: Hakika mataifa mawili kabla yetu yameteremshiwa Kitabu; na sisi tulikuwa hatuna khabari ya waliyo kuwa wakiyasoma. 156

Maelezo ya chini

156 Tumeiteremsha hii Qur'ani ili msipate kutoa udhuru kwa uasi wenu mkasema: Wahyi haukuteremka ila kwa mataifa mawili tu ya kabla yetu, nao ni watu wa Taurati na watu wa Injili. Na sisi hatuna ilimu kabisa ya kusoma vitabu vyao na kufahamu uwongozi uliomo humo.