وَأَنَّ هَٰذَا صِرَٰطِي مُسۡتَقِيمٗا فَٱتَّبِعُوهُۖ وَلَا تَتَّبِعُواْ ٱلسُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمۡ عَن سَبِيلِهِۦۚ ذَٰلِكُمۡ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ ١٥٣
Wa anna hādhā sirātī mustaqīman fattabi'ūhu walā tattabi'us-subula fatafarraqa bikum 'an sabīlihī dhālikum wassākum bihī la'allakum tattaqūn
Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya amekuusieni ili mpate kuchamngu. 153
Maelezo ya chini
153 Wala msiiache Njia niliyo kuwekeeni, kwani hiyo ndiyo Njia Iliyo Nyooka itayo kufikisheni kwenye mafanikio ya duniani na Akhera. Bali ifuateni Njia hii, wala msifuate njia nyingine za upotovu alizo kukatazeni Mwenyezi Mungu, ili msije kufarikiana mkawa makundi makundi na mapande mapande, ya madhehebu na vyama, na mkawa mbali na Njia ya Mwenyezi Mungu iliyo kaa sawa. Mwenyezi Mungu amekuamrisheni kwa amri ya nguvu ili msije mkamkhalifu Yeye.