ثُمَّ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ تَمَامًا عَلَى ٱلَّذِيٓ أَحۡسَنَ وَتَفۡصِيلٗا لِّكُلِّ شَيۡءٖ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ لَّعَلَّهُم بِلِقَآءِ رَبِّهِمۡ يُؤۡمِنُونَ ١٥٤
Thumma ātaynā mūsal-kitāba tamāman 'alal-ladhī ahsana watafsīlal likulli shay'in wahudan warahmatal la'allahum biliqā'i rabbihim yu'minūn
Tena tulimpa Musa Kitabu kwa kumtimizia (neema) aliye fanya wema, na kuwa ni maelezo ya kila kitu, na uwongofu na rehema, ili wapate kuamini mkutano wao na Mola wao Mlezi. 154
Maelezo ya chini
154 Na tulimteremshia Musa Taurati kwa kumtimizia neema mtu aliye simama msimamo mwema katika mambo ya Dini. Na tuliiteremsha kwa kueleza wazi kila jambo katika mafunzo yalio nasibiana na watu wake, na ni uwongofu kwendea Njia iliyo sawa, na rehema kwao kwa kuifuata. Na hayo ni hivyo ili Wana wa Israili waiamini Siku ya kukutana na Mola wao Mlezi, Siku ya Kiyama na kuhisabiwa kwa mambo walio amrishwa kuyafanya.