Surat Al-An'am, aya 146

6:146

وَعَلَى ٱلَّذِينَ هَادُواْ حَرَّمۡنَا كُلَّ ذِي ظُفُرٖۖ وَمِنَ ٱلۡبَقَرِ وَٱلۡغَنَمِ حَرَّمۡنَا عَلَيۡهِمۡ شُحُومَهُمَآ إِلَّا مَا حَمَلَتۡ ظُهُورُهُمَآ أَوِ ٱلۡحَوَايَآ أَوۡ مَا ٱخۡتَلَطَ بِعَظۡمٖۚ ذَٰلِكَ جَزَيۡنَٰهُم بِبَغۡيِهِمۡۖ وَإِنَّا لَصَٰدِقُونَ ١٤٦

Wa'alal-ladhīna hādū harramnā kulla dhī zufurin waminal-baqari wal-ghanami harramnā 'alayhim shuhūmahumā illā mā hamalat zuhūruhumā awil-hawāyā aw makhtalata bi'azmin dhālika jazaynāhum bibaghyihim wa innā lasādiqūn

Na wale walio fuata dini ya Kiyahudi tumewaharimishia kila mwenye kucha. Na katika ng'ombe na kondoo na mbuzi tumewaharimishia shahamu yao, isipo kuwa ile iliyo beba migongo yao au matumbo yao, au iliyo gandamana na mifupa. Tuliwalipa hivyo kwa sababu ya uasi wao. Na bila ya shaka Sisi ndio wasema kweli. 146

Maelezo ya chini

146 Basi hivi ndivyo tulivyo kuharimishieni nyinyi. Na Mayahudi tuliwaharimishia nyama na shahamu na kila kitu cha wenye makucha katika wanyama, kama ngamia na wanyama wawindao. Na katika ng'ombe na mbuzi na kondoo tuliwaharimishia shahamu yake tu, ila shahamu ya mgongoni, au iliyoko matumboni, au iliyo changanyika na mafupa. Na kuharimishwa huku kulikuwa kwa ajili ya kuwatesa tu kwa ajili ya dhulma zao, na kuziachisha nafsi zao waweze kujilinda na matamanio. Na hakika Sisi tunasema kweli katika maneno yetu yote, na miongoni ya hayo ni khabari hii.