فَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل رَّبُّكُمۡ ذُو رَحۡمَةٖ وَٰسِعَةٖ وَلَا يُرَدُّ بَأۡسُهُۥ عَنِ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ ١٤٧
Fa in kaddhabūka faqur rabbukum dhū rahmatin wāsi'atin walā yuraddu ba suhū 'anil-qawmil-mujrimīn
Wakikukanusha basi wewe sema: Mola Mlezi wenu ni Mwenye rehema iliyo enea. Wala haizuiliki adhabu yake kwa watu wakhalifu. 147
Maelezo ya chini
147 Wakanushi wakikukanusha katika haya tuliyo kuletea wahyi, waambie kwa kuwahadharisha: Hakika Mola Mlezi wenu, ambaye anapasa mumuamini Yeye peke yake, na mfuate hukumu zake, ana rehema iliyo enea na kumfikia kila anaye mt'ii, na pia anaye muasi kwa kuwa hafanyi haraka kuwaadhibu. Na lakini haitakikani mghurike na hivyo kuwa rehema yake imeenea kote, kwa sababu adhabu yake haina budi kuwafikia hao wakhalifu.