Surat Al-An'am, aya 138

6:138

وَقَالُواْ هَٰذِهِۦٓ أَنۡعَٰمٞ وَحَرۡثٌ حِجۡرٞ لَّا يَطۡعَمُهَآ إِلَّا مَن نَّشَآءُ بِزَعۡمِهِمۡ وَأَنۡعَٰمٌ حُرِّمَتۡ ظُهُورُهَا وَأَنۡعَٰمٞ لَّا يَذۡكُرُونَ ٱسۡمَ ٱللَّهِ عَلَيۡهَا ٱفۡتِرَآءً عَلَيۡهِۚ سَيَجۡزِيهِم بِمَا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ ١٣٨

Waqālū hādhihī an'āmun waharthun hijrul lā yat'amuhā illā man nashā'u biza'mihim wa an'āmun hurrimat zuhūruhā wa an'āmul lā yadhkurūnasmallāhi 'alayhaftirā'an 'alayhi sayajzīhim bimā kānū yaftarūn

Nao husema: Wanyama hawa na mimea hii ni mwiko. Hawatokula ila wale tuwapendao - kwa madai yao tu. Na wanyama hawa imeharimishwa migongo yao kupandwa. Na wanyama wengine hawalitaji jina la Mwenyezi Mungu juu yao. Wanamzulia uwongo tu Mwenyezi Mungu. Atawalipa kwa hayo wanayo mzulia. 138

Maelezo ya chini

138 Na katika mawazo yao ni kusema kwao: Ngamia hawa, na ng'ombe hawa, na mbuzi na kondoo hawa, na mazao haya ya mimea, ni marfuku. Hayali mtu ila wamtakaye katika utumishi wa masanamu. Hayo ni kwa madai yao ya uwongo, wala hayatokani na Mwenyezi Mungu. Na pia husema: Ngamia hawa wameharimishwa migongo yao, basi hapana ruhusa mtu kuwapanda. Nao juu ya hao hawalitaji jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu wanapo wachinja hao ngamia, na ng'ombe, na mbuzi na kondoo. Na hayo ni kwa kule kumzulia uwongo Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ushirikina wao. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu atawalipa adhabu huko Akhera kwa sababu ya uzushi wao, na kuharimisha kwao vitu ambavyo Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuharimisha.