Surat Al-An'am, aya 130

6:130

يَٰمَعۡشَرَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِ أَلَمۡ يَأۡتِكُمۡ رُسُلٞ مِّنكُمۡ يَقُصُّونَ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتِي وَيُنذِرُونَكُمۡ لِقَآءَ يَوۡمِكُمۡ هَٰذَاۚ قَالُواْ شَهِدۡنَا عَلَىٰٓ أَنفُسِنَاۖ وَغَرَّتۡهُمُ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا وَشَهِدُواْ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ أَنَّهُمۡ كَانُواْ كَٰفِرِينَ ١٣٠

Yāma'sharal-jinni wal-insi alam ya'tikum rusulum minkum yaqussūna 'alaykum āyātī wayundhirūnakum liqā'a yawmikum hādhā qālū shahidnā 'alā anfusinā wagharrathumul-hayawātud-dunyā washahidū 'alā anfusihim annahum kānū kāfirīn

Enyi makundi ya majini na watu! Je, hawakukujieni Mitume kutokana na nyinyi wenyewe wakikubainishieni Aya zangu, na wakikuonyeni mkutano wa Siku yenu hii. Nao watasema: Tumeshuhudia juu ya nafsi zetu. Na yaliwadanganya maisha ya dunia. Nao watajishuhudia wenyewe ya kwamba walikuwa makafiri. 130

Maelezo ya chini

130 Na Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia Siku ya Kiyama: Enyi watu na majini! Mitume wamekujieni wakikutajieni hoja na dalili zilizo wazi, na wakikusomeeni Aya, na wakikuonyeni na mkutano wa Mwenyezi Mungu katika Siku yenu hii. Basi vipi mnakanusha? Nao watajibu: Tunakubali wenyewe madhambi tuliyo yatenda. Na maisha ya kidunia yaliwakhadaa kwa starehe zake, na wakajikiria nafsi zao kuwa hakika wao walikuwa wapinzani.