۞ وَلَوۡ أَنَّنَا نَزَّلۡنَآ إِلَيۡهِمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ وَكَلَّمَهُمُ ٱلۡمَوۡتَىٰ وَحَشَرۡنَا عَلَيۡهِمۡ كُلَّ شَيۡءٖ قُبُلٗا مَّا كَانُواْ لِيُؤۡمِنُوٓاْ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ يَجۡهَلُونَ ١١١
Walaw annanā nazzalnā ilayhimul-malā'ikata wakallamahumul-mawtā wahasharnā 'alayhim kulla shay'in qubulam mā kānū liyu'minū illā an yashā'allāhu walākinna aktharahum yajhalūn
NA LAU kuwa tungeli wateremshia Malaika, na maiti wakazungumza nao, na tukawakusanyia kila kitu mbele yao, bado wasingeli amini, ila Mwenyezi Mungu atake. Lakini wengi wao wamo ujingani. 111
Maelezo ya chini
111 Hakika hao walio apa kuwa ikiwajia Ishara wataiamini, ni waongo. Mwenyezi Mungu anaijua vilivyo imani yao. Lau kuwa sisi tungeli teremsha Malaika wakawaona kwa macho, na maiti wakawasemeza baada ya kufufuliwa makaburini mwao, na kuwakusanyia kila kitu mbele yao kikiwakabili na kuwabainishia haki, bado wasingeli amini ila akipenda Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa waamini. Na wengi hawaitambui Haki wala hawaifuati, kwa sababu nyoyo zao zimesibiwa na upofu wa kijahiliya.