وَأَقۡسَمُواْ بِٱللَّهِ جَهۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡ لَئِن جَآءَتۡهُمۡ ءَايَةٞ لَّيُؤۡمِنُنَّ بِهَاۚ قُلۡ إِنَّمَا ٱلۡأٓيَٰتُ عِندَ ٱللَّهِۖ وَمَا يُشۡعِرُكُمۡ أَنَّهَآ إِذَا جَآءَتۡ لَا يُؤۡمِنُونَ ١٠٩
Wa aqsamū billāhi jahda aymānihim la in jā'athum āyatul layu'minunna bihā qul innamal-āyātu 'indallāhi wamā yush'irukum annahā idhā jā'at lā yu'minūn
Na waliapa kwa Mwenyezi Mungu kwa ukomo wa viapo vyao, kuwa ikiwafikia Ishara wataiamini. Sema: Ishara ziko kwa Mwenyezi Mungu. Na nyinyi hamjui kuwa zitapo kuja hawato amini. 109
Maelezo ya chini
109 Na washirikina waliapa ukomo wa viapo vyao, kuwa ikiwajia Ishara ya kuiona katika Ishara walizo zitaka, basi yakini hiyo itakuwa ni sababu ya kuamini kwao. Sema ewe Nabii: Ishara hizi ziko kwa Mwenyezi Mungu. Yeye peke yake ndiye Mwenye madaraka juu yake hizo ishara. Mimi sina uweza wa hayo. Nyinyi Waumini, hamjui ninayo yajua Mimi. Hata zikiwajia Ishara hizi hawataamini.