Surat Al-An'am, aya 105

6:105

وَكَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ ٱلۡأٓيَٰتِ وَلِيَقُولُواْ دَرَسۡتَ وَلِنُبَيِّنَهُۥ لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ ١٠٥

Wakadhālika nusarriful-āyāti waliyaqūlū darasta walinubayyinahū liqawmin ya'lamūn

Na namna hivyo tunazisarifu Aya, na wao wakwambie: Umesoma. Na ili tuyabainishe kwa watu wanao jua. 105

Maelezo ya chini

105 Na mfano wa uchambuzi kama huu wa pekee katika kueleza dalili za maumbile, ndivyo tunavyo eleza Ishara zetu katika Qur'ani kwa njia namna kwa namna na kwa mbali mbali, ili kusimamisha hoja za kuwashinda hao wapingao. Kwa hivyo wao hawapati ila kuzua uwongo, wakakutuhumu kuwa haya umejifunza kwa watu, wala hayakutoka kwa Mwenyezi Mungu. Nasi tunabainisha haya uliyo teremshiwa, nayo ni Haki isiyo athirika na kipendacho moyo, kwa ajili ya watu ambao wanayo ielewa Haki na wanainyenyekea.