قَدۡ جَآءَكُم بَصَآئِرُ مِن رَّبِّكُمۡۖ فَمَنۡ أَبۡصَرَ فَلِنَفۡسِهِۦۖ وَمَنۡ عَمِيَ فَعَلَيۡهَاۚ وَمَآ أَنَا۠ عَلَيۡكُم بِحَفِيظٖ ١٠٤
Qad jā'akum basā'iru mir rabbikum faman absara falinafsihī waman 'amiya fa'alayhā wamā ana 'alaykum bihafīz
Zimekwisha kukujieni hoja wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anaye ona ni kwa faida yake mwenyewe, na anaye pofuka basi ni khasara yake. Nami si mtunzaji wenu. 104
Maelezo ya chini
104 Ewe Nabii! Waambie watu: Zimekwisha kujieni kutoka kwa Muumba wenu na Mwenye kumiliki mambo yenu yote, hoja na maelezo wazi katika hii Qur'ani. Hizo zinakuangazieni Njia ya Haki. Basi mwenye kunafiika kwazo, manufaa ni yake mwenyewe. Na mwenye kujitenga nazo, basi amejidhuru mwenyewe! Wala mimi si mlinzi wenu, bali mimi ni Mjumbe ninakufikishieni niliyo tumwa kwenu.