۞ لَّئِن لَّمۡ يَنتَهِ ٱلۡمُنَٰفِقُونَ وَٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ وَٱلۡمُرۡجِفُونَ فِي ٱلۡمَدِينَةِ لَنُغۡرِيَنَّكَ بِهِمۡ ثُمَّ لَا يُجَاوِرُونَكَ فِيهَآ إِلَّا قَلِيلٗا ٦٠
Lla il lam yantahil-munāfiqūna walladhīna fī qulūbihim maradun wal-murjifūna fil-madīnati lanughriyannaka bihim thumma lā yujāwirūnaka fīhā illā qalīlā
Kama wanaafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitna katika Madina hawatoacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu. 60
Maelezo ya chini
60 Ninaapa! Ikiwa hawataacha hao wanaafiki, na wenye maradhi katika nyoyo zao, na wanao eneza khabari za uwongo katika Madina, hapana shaka nitakusalitisha juu yao, kisha hawatabakia kuwa karibu yako ila kwa muda mchache tu.