وَلَا تُطِعِ ٱلۡكَٰفِرِينَ وَٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَدَعۡ أَذَىٰهُمۡ وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلٗا ٤٨
Walā tuti'il-kāfirīna wal-munāfiqīna wada' adhāhum watawakkal 'alallāhi wakafā billāhi wakīlā
Wala usiwat'ii makafiri na wanaafiki, na usijali udhia wao. Nawe mtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mtegemewa. 48
Maelezo ya chini
48 Na wala usiwafuate makafiri na wanaafiki, wala usijishughulishe na maudhi yao. Na mfanye Mwenyezi Mungu ndiye Wakili wako wa kumtegemea kukulinda na madhara yao na shari zao. Na Mwenyezi Mungu anakutosha kabisa kuwa ndiye Mtegemewa wa kukukifia na kukukinaisha.