Surat Al-Ahzab, aya 34

33:34

وَٱذۡكُرۡنَ مَا يُتۡلَىٰ فِي بُيُوتِكُنَّ مِنۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ وَٱلۡحِكۡمَةِۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ لَطِيفًا خَبِيرًا ٣٤

Wadhkurna mā yutlā fī buyūtikunna min āyātillāhi wal-hikmati innallāha kāna latīfan khabīrā

Na kumbukeni yasomwayo majumbani mwenu katika Aya za Mwenyezi Mungu na hikima. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mambo ya siri, na Mwenye khabari. 34

Maelezo ya chini

34 Na hifadhini yanayo somwa katika nyumba zenu ya Qur'ani aliyo iteremsha Mwenyezi Mungu, na hikima zilio sawa za Mtume wa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua mambo yalio zama ndani kabisa na ya hakika yake. Basi tahadharini na kwenda kinyume naye na kumuasi Mtume wake.