Surat Al-Ahzab, aya 33

33:33

وَقَرۡنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجۡنَ تَبَرُّجَ ٱلۡجَٰهِلِيَّةِ ٱلۡأُولَىٰۖ وَأَقِمۡنَ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتِينَ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَطِعۡنَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓۚ إِنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيُذۡهِبَ عَنكُمُ ٱلرِّجۡسَ أَهۡلَ ٱلۡبَيۡتِ وَيُطَهِّرَكُمۡ تَطۡهِيرٗا ٣٣

Waqarna fī buyūtikunna walā tabarrajna tabarrujal-jāhiliyyatil-ūlā wa aqimnas-salawāta wa ātīnaz-zakawāta wa ati'nallāha warasūlahū innamā yurīdullāhu liyudhhiba 'ankumur-rijsa ahlal-bayti wayutahhirakum tathīrā

Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani. Na shikeni Swala, na toeni Zaka, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na kukusafisheni baarabara. 33

Maelezo ya chini

33 Na kaeni nyumbani kwenu, wala msitoke ila kwa haja. Wala msidhihirishe uzuri wenu na mapambo yenu kwa wanaume pale mnapo toka, kama walivyo kuwa wakifanya watu wa ujahili wa zamani. Na timizeni Swala kwa ukamilifu, na toeni Zaka, na fuateni amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hakika Mwenyezi Mungu anataka, kwa yote anayo kuamrisheni na kukukatazeni, mpate utukufu na hishima, ili muondokewe na madhambi na maasia, enyi Ahli Baiti Nnabii, Watu wa Nyumba ya Nabii, na akusafisheni kwa usafi usio kuwa na shaka.