مِّنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ رِجَالٞ صَدَقُواْ مَا عَٰهَدُواْ ٱللَّهَ عَلَيۡهِۖ فَمِنۡهُم مَّن قَضَىٰ نَحۡبَهُۥ وَمِنۡهُم مَّن يَنتَظِرُۖ وَمَا بَدَّلُواْ تَبۡدِيلٗا ٢٣
Mminal-mu'minīna rijālun sadaqū mā 'āhadullāha 'alayhi faminhum man qadā nahbahū waminhum man yantaziru wamā baddalū tabdīlā
Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo. 23
Maelezo ya chini
23 Miongoni mwa hawa Waumini wapo watu walio muahidi Mwenyezi Mungu kuwa watasimama imara na Mtume katika vita. Nao wakatimiza ahadi yao. Miongoni mwao wapo walio pata utukufu wa kufa mashahidi, na wengine wamebakia wahai wakingojea nao kupata utukufu huo. Wala hawakuigeuza ahadi ya Mwenyezi Mungu waliyo jikatia juu ya nafsi yao, wala hawakugeuza chochote katika hayo.