Surat Al-Ahzab, aya 20

33:20

يَحۡسَبُونَ ٱلۡأَحۡزَابَ لَمۡ يَذۡهَبُواْۖ وَإِن يَأۡتِ ٱلۡأَحۡزَابُ يَوَدُّواْ لَوۡ أَنَّهُم بَادُونَ فِي ٱلۡأَعۡرَابِ يَسۡـَٔلُونَ عَنۡ أَنۢبَآئِكُمۡۖ وَلَوۡ كَانُواْ فِيكُم مَّا قَٰتَلُوٓاْ إِلَّا قَلِيلٗا ٢٠

Yahsabūnal-ahzāba lam yadhhabū wa in ya'til-ahzābu yawaddū law annahum bādūna fil-a'rābi yas'alūna 'an ambā'ikum walaw kānū fīkum mā qātalū illā qalīlā

Wanafikiri yale makundi ya maadui hayajaondoka. Na yakija hayo makundi watatamani laiti wao wako majangwani pamoja na mabedui, wakiuliza khabari zenu. Na lau wakiwa pamoja nanyi hawapigani ila kidogo tu. 20

Maelezo ya chini

20 Wanadhani hawa wanaafiki kwamba majeshi ya makafiri yaliyo ungana bado yapo mahali pao wanaizinga Madina. Na hayo makundi ya maadui yakirejea tena, watatamani hao woga laiti wangeli kuwa wanaishi pamoja na mabedui huko majangwani wakidondoa khabari zenu. Na lau wakibaki kwenye kambi zao, na wasikimbie, na majeshi mawili yakapambana, basi hata hivyo wasinge pigana pamoja nanyi ila kidogo tu, kama kujionyesha na watajwe kuwa nao walikuwamo.