Surat Yusuf, aya 68

12:68

وَلَمَّا دَخَلُواْ مِنۡ حَيۡثُ أَمَرَهُمۡ أَبُوهُم مَّا كَانَ يُغۡنِي عَنۡهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٍ إِلَّا حَاجَةٗ فِي نَفۡسِ يَعۡقُوبَ قَضَىٰهَاۚ وَإِنَّهُۥ لَذُو عِلۡمٖ لِّمَا عَلَّمۡنَٰهُ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ ٦٨

Walammā dakhalū min haythu amarahum abūhum mā kāna yughnī 'anhum minallāhi min shay'in illā hājatan fī nafsi ya'qūba qadāhā wa innahū ladhū 'ilmil limā 'allamnāhu walākinna aktharan-nāsi lā ya'lamūn

Na walipo ingia kama alivyo waamrisha baba yao, haikuwafaa kitu kwa Mwenyezi Mungu, isipo kuwa ni haja tu iliyo kuwa katika nafsi ya Yaa'qub aliitimiza. Na hakika yeye alikuwa na ilimu kwa sababu tulimfundisha; lakini watu wengi hawajui. 68

Maelezo ya chini

68 Wale vijana wakapokea wasia wa baba yao, wakapitia milango mbali mbali. Wala hayo si kama ndiyo ya kuwazuilia madhara walio kwisha andikiwa na Mwenyezi Mungu! Na Yaa'qub akijua hayo, kwani yeye alikuwa na ilimu tuliyo mfundisha. Lakini wasia wake ulikuwa ni kwa haja aliyo kuwa nayo nafsini mwake tu, nayo ni huruma ya baba kwa wanawe ambayo ameidhihirisha katika huu wasia. Na hakika watu wengi hawana ujuzi kama alio kuwa nao Yaa'qub wakamwachia mambo yao Mwenyezi Mungu awalinde.