Surat Yusuf, aya 67

12:67

وَقَالَ يَٰبَنِيَّ لَا تَدۡخُلُواْ مِنۢ بَابٖ وَٰحِدٖ وَٱدۡخُلُواْ مِنۡ أَبۡوَٰبٖ مُّتَفَرِّقَةٖۖ وَمَآ أُغۡنِي عَنكُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٍۖ إِنِ ٱلۡحُكۡمُ إِلَّا لِلَّهِۖ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُۖ وَعَلَيۡهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُتَوَكِّلُونَ ٦٧

Waqāla yābaniyya lā tadkhulū mim bābin wāhidin wadkhulū min abwābim mutafarriqatin wamā ughnī 'ankum minallāhi min shay'in inil-hukmu illā lillāhi 'alayhi tawakkaltu wa'alayhi falyatawakkalil-mutawakkilūn

Na akasema: Enyi wanangu! Msiingie mlango mmoja, bali ingieni kwa milango mbali mbali. Wala mimi sikufaeni kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Hukumu haiko ila kwa Mwenyezi Mungu tu. Juu yake Yeye mimi nimetegemea, na juu yake Yeye wategemee wanao tegemea. 67

Maelezo ya chini

67 Yaa'qub alitua kwa ahadi ya watoto wake. Kisha huruma ilimpelekea kuwausia kuwa watapo ingia Misri waingie kupita milango mbali mbali, ili watu wasiwapige kijicho, huenda wakadhurika. Akasema: Wala mimi sina uwezo wa kukulindeni na madhara. Kwani mwenye kuzuia madhara ni Mwenyezi Mungu tu, na hukumu ni yake Yeye pekee. Mimi nimemtegemea Yeye, na mambo yangu na yenu yote nimemwachia Yeye. Na juu yake Yeye peke yake wategemee wote wanao tegemeza mambo yao, kwa kumuamini Yeye.