Surat Yusuf, aya 6

12:6

وَكَذَٰلِكَ يَجۡتَبِيكَ رَبُّكَ وَيُعَلِّمُكَ مِن تَأۡوِيلِ ٱلۡأَحَادِيثِ وَيُتِمُّ نِعۡمَتَهُۥ عَلَيۡكَ وَعَلَىٰٓ ءَالِ يَعۡقُوبَ كَمَآ أَتَمَّهَا عَلَىٰٓ أَبَوَيۡكَ مِن قَبۡلُ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡحَٰقَۚ إِنَّ رَبَّكَ عَلِيمٌ حَكِيمٞ ٦

Wakadhālika yajtabīka rabbuka wayu'allimuka min ta'wīlil-ahādīthi wayutimmu ni'matahū 'alayka wa'alā āli ya'qūba kamā atammahā 'alā abawayka min qablu ibrāhīma wa ishāqa inna rabbaka 'alīmun hakīm

Na kadhaalika Mola wako Mlezi atakuteuwa na atakufundisha tafsiri ya mambo. Na atatimiza neema zake juu yako na juu ya ukoo wa Yaa'qub, kama alivyo watimizia hapo zamani baba zako Ibrahim na Is-haq. Hakika Mola wako Mlezi ni Mjuzi Mwenye hikima. 6

Maelezo ya chini

6 Kama ulivyo jiona katika ndoto kuwa ni bwana wa kut'iiwa, mwenye cheo na madaraka, basi Mola wako Mlezi atakuteuwa na atakukhitari, akufunze kufasiri ndoto, kwa kukupa Unabii na Utume, kama hapo zamani, kabla ya baba yako, Yaa'qub, alivyo wafanyia baba zako, Ibrahim na Is-haq. Hakika Mola wako Mlezi ni mwingi wa hikima, basi hakosei. Ni mwingi wa ujuzi, basi humteuwa katika waja wake anaye mjua kuwa anastahili kuteuliwa.