ثُمَّ يَأۡتِي مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ عَامٞ فِيهِ يُغَاثُ ٱلنَّاسُ وَفِيهِ يَعۡصِرُونَ ٤٩
Thumma ya'tī mim ba'di dhālika 'āmun fīhi yughāthun-nāsu wafīhi ya'sirūn
Kisha baada ya haya utakuja mwaka ambao katika mwaka huo watu watasaidiwa, na watakamua. 49
Maelezo ya chini
49 Kisha baada ya miaka hiyo ya ukame utakuja mwaka watu watasaidiwa kwa mvua, na watakamua zabibu na zaituni, na kila cha kukamuliwa.