Surat Yusuf, aya 29

12:29

يُوسُفُ أَعۡرِضۡ عَنۡ هَٰذَاۚ وَٱسۡتَغۡفِرِي لِذَنۢبِكِۖ إِنَّكِ كُنتِ مِنَ ٱلۡخَاطِـِٔينَ ٢٩

Yūsufu a'rid 'an hādhā wastaghfirī lidhambiki innaki kunti minal-khāti'īn

Yusuf! Wachilia mbali haya. Na wewe, mwanamke, omba msamaha kwa dhambi zako. Kwa hakika wewe ni katika walio fanya makosa. 29

Maelezo ya chini

29 Ewe Yusuf wachilia mbali mambo haya, na wewe yafiche wala usiyaseme. Na wewe, mwanamke, omba maghfira kwa dhambi yako. Hapana shaka kuwa wewe ni katika wenye dhambi, wenye kuyakusudia makosa, na kutenda maasi, na kuwasingizia wengine uasi wasio ufanya!