قُلۡ هَٰذِهِۦ سَبِيلِيٓ أَدۡعُوٓاْ إِلَى ٱللَّهِۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا۠ وَمَنِ ٱتَّبَعَنِيۖ وَسُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ ١٠٨
Qul hādhihī sabīlī ad'ū ilallāhi 'alā basīratin ana wamanit-taba'anī wasubhānallāhi wamā ana minal-mushrikīn
Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina. 108
Maelezo ya chini
108 Ewe Muhammad! Wazindue mwisho wa uwezo wako, na waonyeshe hadi ya juhudi yako, uwaambie: Huu ndio Mwendo wangu na Njia yangu. Nawaita watu wafuate Njia ya Mwenyezi Mungu. Na mimi nimethibiti katika hili jambo langu, na kadhalika anayaitia hayo kila mwenye kunifuata na akaiamini sharia yangu. Na namtakasa Mwenyezi Mungu Subhanahu na kila kisicho kuwa laiki yake. Wala mimi simshirikishi Yeye na kitu chochote.