وَمَا يُؤۡمِنُ أَكۡثَرُهُم بِٱللَّهِ إِلَّا وَهُم مُّشۡرِكُونَ ١٠٦
Wamā yu'minu aktharuhum billāhi illā wahum mushrikūn
Na wengi katika wao hawamuamini Mwenyezi Mungu pasina kuwa ni washirikina. 106
Maelezo ya chini
106 Na kati yao wapo wenye kumsadiki Mwenyezi Mungu, wanamkubali kuwa ni Mola Mlezi, na kwamba Yeye ni Muumba wa kila kitu. Lakini imani ya wengi wao haikusimama juu ya msingi madhubuti wa Tawhid! Basi hawaukubali Upweke wa Mwenyezi Mungu kwa njia ya usafi. Lakini katika nafsi zao umo mchanganyiko wa imani unao wapelekea katika njia za washirikina, mapagani.