وَمَا تَسۡـَٔلُهُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا ذِكۡرٞ لِّلۡعَٰلَمِينَ ١٠٤
Wamā tas'aluhum 'alayhi min ajrin in huwa illā dhikrul lil-'ālamīn
Wala wewe huwaombi ujira kwa haya. Hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu wote. 104
Maelezo ya chini
104 Wala hatukusudii kwa hadithi za uwongofu unazo waeleza kuwa ndio upate malipo au manufaa. Ikiwa hawaongoki hawa usiwahuzunikie. Mwenyezi Mungu atawaongoa watu wengineo. Kwani Sisi hatukuwateremshia wao tu peke yao. Na haya si chochote ila ni mawaidha, na mazingatio kwa kila aliye umbwa na Mwenyezi Mungu katika mbingu na ardhi.