ذَٰلِكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلۡغَيۡبِ نُوحِيهِ إِلَيۡكَۖ وَمَا كُنتَ لَدَيۡهِمۡ إِذۡ أَجۡمَعُوٓاْ أَمۡرَهُمۡ وَهُمۡ يَمۡكُرُونَ ١٠٢
Dhālika min ambā'il-ghaybi nūhīhi ilayka wamā kunta ladayhim idh ajma'ū amrahum wahum yamkurūn
Hizi ni katika khabari za ghaibu tulizo kufunulia. Na hukuwa pamoja nao walipo azimia shauri yao, walipo fanya njama zao wakizua vitimbi. 102
Maelezo ya chini
102 Ewe Nabii! Haya tuliyo kusimulia ni katika khabari zilizo pita za kale. Hazikukufikia ila kwa wahyi ulio toka kwetu. Wala wewe hukuwapo pale nduguze Yusuf walipo kuwa wakipanga njama. Wala wewe hukuwa unavijua vitimbi vyao ila kwa kusimuliwa nasi.