إِنَّ ٱلَّذِينَ حَقَّتۡ عَلَيۡهِمۡ كَلِمَتُ رَبِّكَ لَا يُؤۡمِنُونَ ٩٦
Innal-ladhīna haqqat 'alayhim kalimatu rabbika lā yu'minūn
Hakika wale ambao neno la Mola wako Mlezi limekwisha thibitika juu yao, hawataamini, 96
Maelezo ya chini
96 Hakika wale iliyo kwisha pita juu yao hukumu ya kuwa wao ni makafiri, kwa kujuulikana inadi yao na chuki zao, hawatoamini hata ukijihangaisha vipi nafsi yako kuwakinaisha.