Surat Yunus, aya 74

10:74

ثُمَّ بَعَثۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِۦ رُسُلًا إِلَىٰ قَوۡمِهِمۡ فَجَآءُوهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَمَا كَانُواْ لِيُؤۡمِنُواْ بِمَا كَذَّبُواْ بِهِۦ مِن قَبۡلُۚ كَذَٰلِكَ نَطۡبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِ ٱلۡمُعۡتَدِينَ ٧٤

Thumma ba'athnā mim ba'dihī rusulan ilā qawmihim fajā'ūhum bil-bayyināti famā kānū liyu'minū bimā kaddhabū bihī min qablu kadhālika natba'u 'alā qulūbil-mu'tadīn

Kisha baada yake tukawatuma Mitume kwa watu wao. Nao wakawajia kwa Ishara zilizo wazi. Lakini hawakuwa wenye kuyaamini waliyo yakanusha kabla yake. Ndio kama hivyo tunapiga muhuri juu ya nyoyo za warukao mipaka. 74

Maelezo ya chini

74 Baada ya Nuhu tuliwatuma Mitume wengine wakilingania Tawhid, Upweke wa Mwenyezi Mungu, wakibashiria kheri na wakionya, na wakiungwa mkono na miujiza yenye kuonyesha ukweli wao. Watu wao wakawakanya kama walivyo kanya kaumu ya Nuhu. Haukuwa mwendo wa wapinzani kuwa wat'iifu, kwa sababu kule kukadhbisha kwao kulikuwa ni mbele kuliko kuzingatia na kupima. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu alipiga muhuri wa upotovu juu ya nyoyo za wale ambao mtindo wao ni kuzifanyia uadui hakika na Ishara zilizo wazi!