Surat Yunus, aya 75

10:75

ثُمَّ بَعَثۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِم مُّوسَىٰ وَهَٰرُونَ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ بِـَٔايَٰتِنَا فَٱسۡتَكۡبَرُواْ وَكَانُواْ قَوۡمٗا مُّجۡرِمِينَ ٧٥

Thumma ba'athnā mim ba'dihim mūsā wahārūna ilā fir'awna wamala'ihī bi'āyātinā fastakbarū wakānū qawmam mujrimīn

Kisha baada yao tukamtuma Musa na Haruni kwa Firauni na waheshimiwa wake, kwa Ishara zetu. Wakajivuna, na wakawa watu wakosefu. 75

Maelezo ya chini

75 Kisha baada yao tulimtuma Musa na ndugu yake Haruni wende kwa Firauni, mfalme wa Misri na watu wake wakuu makhsusi, kuwaita wamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake. Nao waliungwa mkono na hoja zenye nguvu. Firauni na kaumu yake walitakabari wakakataa kuitikia wito wa Musa na Haruni. Kwa kukataa kwao huko wakawa wamefanya makosa makubwa na dhambi.