Surat Yunus, aya 59

10:59

قُلۡ أَرَءَيۡتُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ لَكُم مِّن رِّزۡقٖ فَجَعَلۡتُم مِّنۡهُ حَرَامٗا وَحَلَٰلٗا قُلۡ ءَآللَّهُ أَذِنَ لَكُمۡۖ أَمۡ عَلَى ٱللَّهِ تَفۡتَرُونَ ٥٩

Qul ara'aytum mā anzalallāhu lakum mir rizqin faja'altum minhu harāman wahalālan qul āllahu adhina lakum am 'alallāhi taftarūn

Sema: je, mwaonaje zile rizki alizo kutemshieni Mwenyezi Mungu nanyi makafanya katika hizo nyingine haramu na nyingine halali Sema: je, Mwenyezi Mungu amekuruhusuni au mnamzulia Mwenyezi Mungu tu. 59

Maelezo ya chini

59 Ewe Mtume! Waambie makafiri walio pewa baadhi ya starehe za duniani: Niambieni khabari ya vyakula vizuri vya halali alivyo kuruzukuni Mwenyezi Mungu, mkajifanya wenyewe ni watungaji sharia, mkahalalisha vingine na mkaharimisha vingine, bila ya kufuata Sharia ya Mwenyezi Mungu! Hakika Mwenyezi Mungu hakukupeni ruhusa mfanye hayo, bali nyinyi mnamzulia uwongo Mwenyezi Mungu.