Surat Yunus, aya 54

10:54

وَلَوۡ أَنَّ لِكُلِّ نَفۡسٖ ظَلَمَتۡ مَا فِي ٱلۡأَرۡضِ لَٱفۡتَدَتۡ بِهِۦۗ وَأَسَرُّواْ ٱلنَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُاْ ٱلۡعَذَابَۖ وَقُضِيَ بَيۡنَهُم بِٱلۡقِسۡطِ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ ٥٤

Walaw anna likulli nafsin zalamat mā fil-ardi laftadat bihī wa asarrun-nadāmata lammā ra'awul-'adhāba waqudiya baynahum bil-qisti wahum lā yuzlamūn

Na lau kuwa kila nafsi iliyo dhulumu inamiliki kila kiliomo duniani,bila ya shaka ingeli toa vyote kujikombolea. Na watakapo iona adhabu wataficha majuto. Na patahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatadhulumiwa. 54

Maelezo ya chini

54 Na lau kuwa vitu vyote viliomo duniani ni mali ya kila nafsi iliyo dhulumu kwa ushirikina na kukanusha, ingeli vitoa fidia kwa adhabu itayo wakabili Siku ya Kiyama, na ambayo wataviona vitisho vyake. Na hapo basi majuto na masikitiko yatawajaa nyoyoni mwao kwa kutoweza kuyatamka, na kwa fazaa itayo wapata kwa kuiona adhabu! Na hukumu ya Mwenyezi Mungu itapita juu yao kwa uadilifu, na wala hawatodhulumiwa katika malipo hayo, kwani hayo ni matokeo ya waliyo yatenda duniani!