Surat Yunus, aya 53

10:53

۞ وَيَسۡتَنۢبِـُٔونَكَ أَحَقٌّ هُوَۖ قُلۡ إِي وَرَبِّيٓ إِنَّهُۥ لَحَقّٞۖ وَمَآ أَنتُم بِمُعۡجِزِينَ ٥٣

Wayastambi'ūnaka ahaqqun huwa qul ī warabbī innahū lahaqqun wamā antum bimu'jizīn

Na wanakuuliza: Je! Ni kweli hayo? Sema: Ehe! Naapa kwa Mola wangu Mlezi! Hakika hayo ni kweli, na wala nyinyi hamshindi! 53

Maelezo ya chini

53 Na makafiri, kwa njia ya kejeli na kukataa, wanakutaka wewe, Mtume, uwaambie hivyo ni kweli hayo uliyo yaleta katika Qur'ani na khabari za kufufuliwa, na adhabu? Waambie: Naam! Kwa haki ya Muumba wangu aliye niumba, hakika hayo yatakuwa bila ya shaka yoyote. Wala nyinyi hamtoshinda wala hamwezi kuzuia adhabu aitakayo Mwenyezi Mungu kukuleteeni.