وَلَا تَدۡعُ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَۖ فَإِن فَعَلۡتَ فَإِنَّكَ إِذٗا مِّنَ ٱلظَّٰلِمِينَ ١٠٦
Walā tad'u min dūnillāhi mā lā yanfa'uka walā yadurruka fa in fa'alta fa innaka idham minaz-zālimīn
Na wala usiwaombe wasio kuwa Mwenyezi Mungu ambao hawakufai kitu wala hawakudhuru. Ukifanya hivyo basi utakuwa miongoni mwa walio dhulumu. 106
Maelezo ya chini
106 Wala usimkimbilie kwa kumwomba na kumuabudu yeyote asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Hao hawakuletei manufaa wala madhara. Ukifanya hayo inakuwa umekwisha ingia miongoni mwa washirikina walio dhulumu. Na anayo katazwa Nabii, ndio wanakatazwa umma wake wote. Na hivyo ndio ukomo wa kukanya. Kwani kumkanya ambaye hayumkiniki kutenda anacho kanywa, ndio hadi ya kukanya.