Surat Yasin, aya 62

36:62

وَلَقَدۡ أَضَلَّ مِنكُمۡ جِبِلّٗا كَثِيرًاۖ أَفَلَمۡ تَكُونُواْ تَعۡقِلُونَ ٦٢

Walaqad adalla minkum jibillan kathīran afalam takūnū ta'qilūn

Na bila ya shaka yeye amekwisha lipoteza kundi kubwa miongoni mwenu. Je, hamkuwa mkifikiri? 62

Maelezo ya chini

62 Na Shetani amewapotoa viumbe wengi kati yenu. Nyinyi mmeghafilika na hayo. Basi hamkuwa mkifikiri mlipo mt'ii yeye?