Surat Yasin, aya 13

36:13

وَٱضۡرِبۡ لَهُم مَّثَلًا أَصۡحَٰبَ ٱلۡقَرۡيَةِ إِذۡ جَآءَهَا ٱلۡمُرۡسَلُونَ ١٣

Wadrib lahum mathalan ashābal-qaryati idh jā'ahal-mursalūn

Na wapigie mfano wa wakaazi wa mji walipo wafikia walio tumwa. 13

Maelezo ya chini

13 Ewe Nabii! Watajie watu wako kisa cha mji mmoja Kwani hicho ni kama kisa chao. Waliwaendea Wajumbe walio tumwa ili wawahidi (awaongoze). Baadhi wa wafasiri wanasema mji huo ni Antiokia.