Surat Sad, aya 64

38:64

إِنَّ ذَٰلِكَ لَحَقّٞ تَخَاصُمُ أَهۡلِ ٱلنَّارِ ٦٤

Inna dhālika lahaqqun takhāsumu ahlin-nār

Hakika hayo bila ya shaka ndiyo makhasimiano ya watu wa Motoni. 64

Maelezo ya chini

64 Hakika hayo tuliyo yataja ya hadithi ya watu wa Motoni ni kweli ambayo haina budi kutokea, nayo ni ya kugombana kwa watu wa Motoni wao kwa wao.