Surat Sad, aya 49

38:49

هَٰذَا ذِكۡرٞۚ وَإِنَّ لِلۡمُتَّقِينَ لَحُسۡنَ مَـَٔابٖ ٤٩

Hādhā dhikrun wa inna lil-muttaqīna lahusna ma'āb

Huu ni ukumbusho. Na hakika wachamngu wana marudio mazuri. 49

Maelezo ya chini

49 Haya tuliyo kusimulia ni khabari za baadhi ya Mitume ili kukukumbusha wewe na kuwakumbusha watu wako. Na hakika wachamngu walio jikinga na kumuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu watapata marejeo mazuri na natija njema.