۞ قُلۡ إِنَّمَآ أَعِظُكُم بِوَٰحِدَةٍۖ أَن تَقُومُواْ لِلَّهِ مَثۡنَىٰ وَفُرَٰدَىٰ ثُمَّ تَتَفَكَّرُواْۚ مَا بِصَاحِبِكُم مِّن جِنَّةٍۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا نَذِيرٞ لَّكُم بَيۡنَ يَدَيۡ عَذَابٖ شَدِيدٖ ٤٦
Qul innamā a'izukum biwāhidatin an taqūmū lillāhi mathnā wafurādā thumma tatafakkarū mā bisāhibikum min jinnatin in huwa illā nadhīrul lakum bayna yaday 'adhābin shadīd
Sema: Mimi nakunasihini kwa jambo moja tu - ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili-wawili na mmoja-mmoja; kisha mfikiri. Mwenzenu huyu hana wazimu. Yeye si chochote ila ni Mwonyaji kwenu kabla ya kufika adhabu kali. 46
Maelezo ya chini
46 Waambie: Mimi nakuamrisheni jambo moja tu - Msimame kwa ikhlasi ya kumtakasia Mwenyezi Mungu muache kufuata mitindo yenu ya zamani - katika kuchungua kwa kumsafia niya Mwenyezi Mungu, mkigawika wawili-wawili, au mmoja-mmoja, muangalie kwa uadilifu na insafu. Kisha mfikiri khabari ya huyu mwenzenu, Muhammad, ambaye mmeishi naye na mnajua kuwa akili yake ni timamu. Huyu hana wazimu kwa kuliingia jambo hili. Yeye huyu si chochote ila ni Mwonyaji kwenu, anakuhadharisheni msije mkapata adhabu kali inayo kukabilini mbele yenu.