Surat Saba, aya 27

34:27

قُلۡ أَرُونِيَ ٱلَّذِينَ أَلۡحَقۡتُم بِهِۦ شُرَكَآءَۖ كَلَّاۚ بَلۡ هُوَ ٱللَّهُ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ ٢٧

Qul arūniyal-ladhīna alhaqtum bihī shurakā'a kallā bal huwallāhul-'azīzul-hakīm

Sema: Nionyesheni mlio waunganisha naye kuwa washirika. Hasha! Bali Yeye ndiye Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu, Mwenye hikima. 27

Maelezo ya chini

27 Waambie: Nionyesheni hao mlio waunganisha na Mwenyezi Mungu kwa kustahiki kuabudiwa, mnao dai kuwa ni miungu wa shirika na Yeye. Yeye hana mshirika, bali Yeye ndiye Mwenyezi Mungu Mwenye kushinda kila kitu, Mwenye hikima katika kupanga kwake na kuendesha kwake.