Surat Saba, aya 16

34:16

فَأَعۡرَضُواْ فَأَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ سَيۡلَ ٱلۡعَرِمِ وَبَدَّلۡنَٰهُم بِجَنَّتَيۡهِمۡ جَنَّتَيۡنِ ذَوَاتَيۡ أُكُلٍ خَمۡطٖ وَأَثۡلٖ وَشَيۡءٖ مِّن سِدۡرٖ قَلِيلٖ ١٦

Fa a'radū fa arsalnā 'alayhim saylal-'arimi wabaddalnāhum bijannatayhim jannatayni dhawātay ukulin khamtin wa athlin washay'im min sidrin qalīl

Lakini wakaacha. Tukawapelekea mafuriko makubwa, na tukawabadilishia badala ya bustani zao hizo kwa bustani nyengine zenye matunda makali machungu, na mivinje, na kidogo katika miti ya kunazi. 16

Maelezo ya chini

16 Lakini wao waliacha kushukuru neema, na wakawa maisha yao ya kiburi. Tukawafungulia mafuriko ya nguvu yaliyo tokea baada ya kupasuka kuta za mahodhi, yakateketeza mabustani yao. Tukawabadilishia badala ya bustani zao mbili zile zenye matunda mazuri, zikawa nyengine mbili zenye matunda machungu, na miti isiyo kuwa na matunda, na mikunazi kidogo isiyo toa hamu. Hili liitwalo "Hodhi" la maji ya mvua kubwa au "Hodhi la Ma`arib" ni kubwa kuliko mahodhi yote ya Yaman. Hodhi hili linaweza kubadilisha ardhi kavu ya kiasi ya maili 300 ya mraba ikawa yenye rutba na mashamba. Na dalili ya hayo ni hizo bustani mbili zilizo tajwa. Wanazuoni wa taarikh (historia) wanakhitalifiana katika ujenzi wa hilo hodhi kuu. Vile vile zipo kauli mbali mbali kukhusu kubomoka kwake.