Surat Saba, aya 17

34:17

ذَٰلِكَ جَزَيۡنَٰهُم بِمَا كَفَرُواْۖ وَهَلۡ نُجَٰزِيٓ إِلَّا ٱلۡكَفُورَ ١٧

Dhālika jazaynāhum bimā kafarū wahal nujāzī illal-kafūr

Hayo tuliwalipa kwa sababu ya walivyo kufuru. Nasi kwani tunamuadhibu isipo kuwa anaye kufuru? 17

Maelezo ya chini

17 Hayo ndiyo malipo tuliyo walipa kwa kufuru zao kuzikufuru neema na kuto zishukuru. Na kwani Sisi tunamuadhibu kwa adhabu hii kali yeyote yule ila aliye kuwa mwingi wa kumkufuru Mwenyezi Mungu na fadhila zake?