Rabbir-hamhuma

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

۞ وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّآ إِيَّاهُ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَٰنًاۚ إِمَّا يَبۡلُغَنَّ عِندَكَ ٱلۡكِبَرَ أَحَدُهُمَآ أَوۡ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَآ أُفّٖ وَلَا تَنۡهَرۡهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوۡلٗا كَرِيمٗا ٢٣

Waqadā rabbuka allā ta'budū illā iyyāhu wabil-wālidayni ihsānan immā yablughanna 'indakal-kibara ahaduhumā aw kilāhumā falā taqul lahumā uffin walā tanharhumā waqul lahumā qawlan karīmā

Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. 23

Maelezo ya chini

23 Na Mola wako Mlezi amehukumu kuwa msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye. Na pia muwafanyie wema kwa ukamilifu wazazi wenu wawili. Na hao, au mmoja wao, wakifikilia kwako hali ya unyonge na mwisho wa umri wao, basi lisikutoke tamko la kuchoka nao au kuudhika kwa yanayo kupata kutokana nao. Wala usiwahamakie. Na nena nao maneno mazuri, laini, yenye kuwaonyesha ihsani na kuwahishimu.

وَٱخۡفِضۡ لَهُمَا جَنَاحَ ٱلذُّلِّ مِنَ ٱلرَّحۡمَةِ وَقُل رَّبِّ ٱرۡحَمۡهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرٗا ٢٤

Wakhfid lahumā janāhadh-dhulli minar-rahmati waqur rabbirhamhumā kamā rabbayānī saghīrā

Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni. 24

Maelezo ya chini

24 Na wafanyie upole, na wanyenyekee kwa kuwaonea huruma, na uwaombee: Ewe Mola Mlezi! Warehemu wote wawili, kama walivyo nifanyia huruma walipo nilea utotoni.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Soma Surat Al-Isra yote

Maswali

Rabbir-hamhuma iko wapi katika Qur'ani?

Rabbir-hamhuma iko katika Surat Al-Isra, 17:23-24.