ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ ٱتَّبَعُواْ مَآ أَسۡخَطَ ٱللَّهَ وَكَرِهُواْ رِضۡوَٰنَهُۥ فَأَحۡبَطَ أَعۡمَٰلَهُمۡ ٢٨
Dhālika bi annahumut-taba'ū mā askhatallāha wakarihū ridwānahū fa ahbata a'mālahum
Hayo ni kwa sababu wao waliyafuata yaliyo mchukiza Mwenyezi Mungu na wakachukia yanayo mridhisha, basi akaviangusha vitendo vyao. 28
Maelezo ya chini
28 Kufishwa namna hiyo ya kutisha katika hali hiyo ni kwa kuwa hakika wao waliufuata upotovu ulio mkasirisha Mwenyezi Mungu, na wakaichukia Haki inayo mpendeza Mwenyezi Mungu. Basi akayabat'ilisha waliyo yatenda.